Wewe ndiwe Baba
Wewe ndiwe Mungu
Wewe ndiwe Baba
Usikie kilio chao
Wengine walia mavazi
Wengine walia chakula
Wengine walia kulala
Wengine walia msaada
Wasaidie
Eh he, Wasaidie
Oh, Wasaidie
Eh, Wasaidie
Enyi wazazi wa kambo
Msiwatese yatima
Enyi wazazi wa kambo
Msiwatese yatima
Nao ni watu, mbele za Mungu
Tena wana haki, mbele za Mungu
Msiwatese!
Wanalia, ye ye ye
Eh Mungu, sikia kilio chao!
Hawana baba wala mama
Ee Bwana, wasaidie
Wewe ndiwe msaada wao
Ee Bwana, wasaidie
Wameumizwa sana na maneno ya watu
Wameumizwa sana na maneno ya Walimwengu
Ondoa
Ondoa uchungu mioyoni mwao
Ondoa mawazo mioyoni mwao
Ondoa mikwasi mioyoni mwao
Ondoa hasira mioyoni mwao
Walikula vizuri
Leo wala majalalani
Walilala pazuri
Leo walala mitaroni
Mali zao mmechukua ninyi ndugu zao
Wakija kuomba chakula, mwawanyima
Wakija kuomba
Mwawafukuza kama mbwa
Kuna siku, watoto
Wenu wataitwa yatima
Na watateswa kama mlivyowatesa
Ee Mungu, watazame yatima
Watie nguvu, wasikate tamaa
Kuna siku, watoto wenu wataitwa yatima
Na watateswa kama mlivyowatesa
Wanalia, ye ye ye
Eh Mungu, sikia kilio chao!
Yesu, naomba unitazame mimi yatima
Maana mama ameniacha
Walikuwepo nilidhamimiwa sana
Lakini kwa sasa, dhamani yangu haipo tena
Nisaidie, ewe Yesu
Tunapokwenda, wewe ndiwe kimbilio
Kwanini mimi, kwanini mimi niitwe yatima?