Chorus
Masikini pendo langu-layumba yumba la katika
Nisitiri mola wangu-nisije ni kaadhirika
Verse 1
Nisikizani makini-kisa cha huyu fatani
Ni bora ni kwambiyeni-muyajuwe kwa yakini
Nina teseka moyoni-kijana ni mashakani
Chorus
Verse 2
Ni mengi nilo kusanya-bila moyo kuyapinga
Watu wa kanisengenya-kwa dhiki ilo nizonga
Kumbe yote ni ngafanya-aniona ni mjinga
Chorus
Verse 3
Ataka kuni twaliya-na hazingatii viita
Mwerevu ni yeye piya-ajiona amepata
Ndoa yetu bila haya-meifanya ya utata
Chorus
Verse 4
Mwisho naomba sahali-yote yashe kwa amani
Sito jifanya fedhuli-zngatiyeni wendani
Mapenzi ni ya wawili-watatu ni shaitwani
Chorus
End