Chorus
Habari zangu unazo-kumbe kunguni mtu
Habari zako sinazo-elewa kunguni mtu.2x
Verse 1
Unayataka ya watu-kuya fuata asilani
Nawe kamwe huna utu-thamani yako ni duni
Huto ni tambiia katu-we ni sawa na kunguni
Nani aliye kutwika-aje leo akutuwe
Mwisho wako umefika-ukaye na utambuwe
Chorus
Verse 2
Utaliya na kununa-hapa ndo mwanzo na anza
Naja kuku paka hina-upate kutu pendeza
Utani kwangu hamna -ni bure ntakuliza
Ukome tena ukome -mimi si saizi yako
Nenda zako ukorome -asie kujua kikoko
Kila mtu umuseme -hiyo ndo faida yako
Chorus
Verse 3
Mtu ni kuwa na haya -mabaya ku yaepuka
Wala si wewe malaya -uonaye wa mtaka
Kuzua haya na haya -amani ikatoweka
Arabuni na ulaya -kwote una kashifika
Mfitini uso haya -kwangu nini unataka
Nini ni mekukuseya -wapita ukini baka
Chorus
End